Nahodha wa Yanga, Lamine Moro amesema afya yake imeimarika na mashabiki watarajie kumuona kwenye ubora wake wakati michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara duru ya pili itakaporejea itakapoendelea


Moro anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati, alikosa michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo Yanga waliibuka mabingwa baada ya kupewa ruhusa kurejea kwao nchini Ghana kuiona familia yake


Aidha Moro akiwa Ghana, aliendelea na matibabu ya jeraha la goti ambalo limekuwa likimsumbua mara kwa mara


"Kwa sasa ni mzima wa afya njema na nipo tayari kuitumikia timu yangu, unajua nilikuwa kwenye kipindi kigumu nilikuwa nasumbuliwa na majeraha sehemu ya mguu lakini baada ya kupata matibabu naona nipo vizuri na madaktari wameniruhusu kufanya mazoezi," alisema.


Moro amewataka mashabiki watarajie makubwa kwenye michezo iliyosalia kwani wachezaji wote wa klabu hiyo wanaendelea kufanya mazoezi makali kuandaa na mzunguko wa pili


Alisema akiwa kiongozi wa wachezaji atawahamasisha wenzake kucheza kwa kujituma kuisaidia timu na kuwafanya mashabiki wafurahi wakati wote


Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 44 katika michezo 18, ikishinda mechi 13, sare tano na inaendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo tangu ligi ya msimu huu ianze.


 Chikwende alikuwepo katika kikosi cha Platinums kilichotolewa na Simba kabla ya kutinga hatua za makundi.

INAWEZEKANA ikawa ni habari mbaya kwa mashabiki wa Simba baada ya kusikia winga wao machachari, Perfect Chikwende kutokuwa sehemu ya wachezaji watakaosafiri kwenda nchini DR Congo kucheza mechi ya hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.


Simba inaondoka leo, huku mchezaji huyo akikosekana kutokana na awali tayari alishacheza Ligi hiyo akiwa na kikosi cha FC Platinums.


Ikumbukwe kwamba katika hatua ya awali, Chikwende alicheza kwenye mchezo wa FC Platinums dhidi ya Simba na katika mchezo wa kwanza alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 uliopigwa nchini Zimbabwe.


Platinums licha ya kupata ushindi katika mchezo wa kwanza, walipokuja katika mchezo wa marudiano walifunga 4-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa na Platinums walitolewa na Simba waliingia katika hatua ya makundi.


Baada ya mechi hiyo Simba waliwekeza nguvu kuhakikisha wanaidaka saini ya mchezaji huyo na walifanikiwa kumpa mkataba wa miaka miwili.


 -Kocha wa zamani wa vilabu vya Stade Reims πŸ‡¨πŸ‡΅, Angers πŸ‡¨πŸ‡΅, Simba SC πŸ‡ΉπŸ‡Ώ, AC Leopards πŸ‡¨πŸ‡¬ na Black Leopards πŸ‡ΏπŸ‡¦, Patrick Aussems ametambulishwa na klabu ya AFC Leopards πŸ‡°πŸ‡ͺ kama kocha mkuu mpya wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Kenya.


 KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema; “Tuna mechi 16 ili kumaliza msimu, katika mechi hizo tunatafuta pointi 48, hizi ni pointi nyingi sana katika Ligi yenye ushindani, sio kwa Yanga tu, hata Simba ambayo tunachuana nayo kwa karibu.”


Kaze alisema timu kama Azam na Biashara pia zina nafasi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa japo mashabiki wanaona zina pointi chache kulinganisha na za Simba au Yanga lakini yeye na vijana wake wanajua cha kufanya.


Biashara ni ya nne katika msimamo ikiwa na pointi 29 na Azam ina pointi 33 ikiwa ya tatu katika msimamo zote zina mechi 16 mkononi.


“Katika timu mechi 16 ni nyingi sana, japo lengo letu ni kuzishinda zote, ndiyo sababu tumeweka mikakati kila mechi kucheza kama fainali.


“Tunafanya hivi ili mwisho wa msimu tuone tumepata nini, kwani unaweza kucheza na kushinda mechi zote halafu ukakosa kile ambacho timu inakitarajia ikipate mwishoni mwa msimu,” alisema Kaze ambaye ni raia wa Burundi.


Kauli ya Kaze ni kama iko vichwani mwa mashabiki wa Yanga huko mitandaoni ambao wanawakebehi watani zao Simba kwamba hivi sasa kila mtu ashinde mechi zake zote ili mwishoni waone nani ataibuka bingwa.


 STAA mpya wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wala hawapaswi kupaniki na maneno ya mitandaoni kwani wao wachezaji wanajua nini cha kufanya.


Saido ambaye ni raia wa Burundi ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara na Yanga. Wengine ni Mrundi mwenzie, Fiston Abdul Razak na mzawa, Dickson Job.


Straika huyo mzoefu na mechi kubwa amewasisitiza mashabiki wa Yanga kwamba mchezaji kutofunga siku moja isiwatishe bali waangalie ubora wake uwanjani na tachi zake zilivyo na macho na madhara makubwa.


“Watu wasivunjike moyo kwa matokeo ya mechi ya kirafiki, tutafanya vizuri kwenye mechi ijayo mbele yetu.Mashabiki wazidi kutusapoti sisi kila mechi kwetu itakuwa kama fainali,tutatumia akili na nguvu zetu zote kufikia kwenye malengo ambayo tunayahitaji,”alisema.


Kuhusu hali yake ya kiafya na kama atacheza mechi na Mbeya City alisema anaendelea vizuri na kadri siku zinavyoelekea atajua kama atacheza.


Ingawa Kocha wake, Cedrick Kaze alisema jana kwamba uwezekano wa kucheza Saido kwenye mechi ya wikiendi dhidi ya Mbeya ni hamsini kwa hamsini lakini kikosi chake kina wachezaji wengi wa kuamua matokeo.


 Kwa Tanzania wasanii waliokuwa wametajwa katika tuzo hizo ni Zuchu, Diamond Platnumz, Harmonize na kundi la Rostam.

Sherehe za utoaji tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2021 ambazo zilipangwa kufanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala zimeahirishwa.


Waandaaji tuzo hizo walitangaza jambo hilo jana Alhamisi Februri 4, 2012 kupitia mtandaao wao wa Twitter ambapo sherehe hiyo ilipaswa kufanyika Februari 20, 2021.


Kwa Tanzania wasanii waliokuwa wametajwa katika tuzo hizo ni msanii wa Bongo Fleva Zuchu aliyekuwa akiwania kipengele cha msanii chipukizi,  Diamond Platanumz aliyekuwa akiwania kipengele cha  msanii bora wa mwaka show kali kipindi cha  ‘lockdown’,


Wengine ni Harmonize aliyekuwa akiwania kipingele cha msanii bora wa kiume na Rostam walikuwa wakiwania kipengele cha kundi bora la mwaka.


Hata hivyo pamoja na tangazo hilo la kuahirishwa, MTV haikutoa sababu zozote za kwa nini wameamua  kukufanya hivyo.


Kufanyika kwa tuzo hizo Uganda,, ilikuwa ndio iwe mara ya kwanza kufanyika nchini humo na mara ya pili kufanyika katika  nchi za Afrika Mashariki.


 Siku chache baada ya msanii kutoka lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny, kuachia albamu ya ‘The sound for Africa’ siku tano zilizopita sasa ni zamu ya Mbosso.

Mbosso ametangaza hilo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kwa kuandika’13th March Definition of love’.

Albamu hii itakuwa ya kwanza kwa msanii huyo kuitoa tangu alivyosainiwa katika lebo hiyo mwaka 2018 baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto ambalo alikuwa akifanya nalo kazi.

Tangu akiwa WCB ameshaachia vibao mbalimbali ikiwemo Watakubali, Nadekezwa, Alele,Maajabu, Sonona, Tamba,Nimekuozea,Ate,Nyota na sasa akitamba na kibao cha Fall.

Ujio wa abamu hii kwa mara ya kwanza  msanii huyo alitangaza siku tatu zilizopita ambapo hata hivyo hakutaja tarehe zaidi ya kuwataka watu kutembelea kwenye youtube yake.

Ukiachilia mbali Mbosso ni kama WCB hapapoi kwani msanii mwingine kutoka lebo hiyo, Lavalava ametangaza ujio wa EP yake ambayo anatarajia kuiachia rasmi siku ya sikuu ya ‘Wapendanao’ Februari 14, 2021.