Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 215, waliofanya udanganyifu katika upimaji wa mitihani hiyo, ambapo Darasa la Nne watahiniwa 77 wamefutiwa matokeo, kidato cha pili ni 63 na watahiniwa 75 wa kidato cha Nne.
"Kidato cha Nne somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili asilimia 94.83 likifuatiwa na Chemistry asilimia 87. 09 nafasi ya tatu ni Kingereza kwa asilimia 73.55 na Hisabati ikishika mkia kwa asilimia 20.12"- Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dkt Charles Msonde
0 Comments:
Post a Comment