Ikiwa hajatimiza hata mwaka tangu aliposainiwa na lebo ya WCB, Zuchu amekuwa moto wa kuotea mbali ambapo sasa watu wanaonyesha kutaka kufanya naye kazi ikiwemo kuwa balozi wao.
Msanii kutoka lebo ya WCB, aliyopo juu kwa sasa katika tasnia ya muziki, Zuhura Othuman maarufu kwa jina la Zuchu, nyota yake inazidi kung’ara baada ya kulamba shavu jingine la ubalozi.
Ikiwa hajatimiza hata mwaka tangu aliposainiwa na lebo ya WCB, Zuchu amekuwa moto wa kuotea mbali ambapo sasa watu wanaonyesha kutaka kufanya naye kazi ikiwemo kuwa balozi wao.
Msanii huyo anayetesa kwa sasa na kibao cha ‘sukari’ jana kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameeleza kutangazwa kwake kuwa balozi wa utalii visiwani Zanzibar.
Katika ukurasa wake huo ameandika” Nina furaha kubwa sana kutangazwa rasmi kuwa balozi wa utalii Zanzibar 2021.
“Shukurani zangu za dhati ziende kwa serikali yetu ya Zanzibar ikiongozwa na Rais Hussein Mwinyi na kwenye Wizara ya Utalii ikiongozwa na Waziri Lela Muhamed Musa(Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale).Mwaka
2021 utakuwa mwaka wa kazi.
Ubalozi huu wa Zuchu, unakuwa wa pili, kwani tayari ni balozi wa kampuni ya Rasta ya Darling.
Hatua hii inamfanya kuwaacha mbali wasanii Lavalava na Queen Darleen ambao wana muda murefu katika lebo hiyo, lakini hawajawahi kuwa mabalozi wa bidhaa wala huduma yeyote hadi sasa.
Tangu Zuchu atue WCB, tayari ameshaachia nyimbo 12 kati ya hizo saba zikiwa katika EP yake ya ‘Am Zuchu’ aliyoiachia Aprili mwaka jana.
Nyimbo hizo ni pamoja na Nisamehe, Wana, Raha, Kwaru, Hakuna Kulala, Mauzauza , Ashua Linawachoma na Cheche alizomshirikisha Diamond Platnumz.
Nyingine ni Hasara, Nobody aliyomshirikisha msanii kutoka nchini Nigeria, Joeboy na Sukari wimbo ambao unafanya vizuri kwa sasa tangu alipouachia wiki mbili zilizopita.
0 Comments:
Post a Comment