Lamine moro nipo fiti kwa mzunguko wa pili


 Nahodha wa Yanga, Lamine Moro amesema afya yake imeimarika na mashabiki watarajie kumuona kwenye ubora wake wakati michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara duru ya pili itakaporejea itakapoendelea


Moro anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati, alikosa michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo Yanga waliibuka mabingwa baada ya kupewa ruhusa kurejea kwao nchini Ghana kuiona familia yake


Aidha Moro akiwa Ghana, aliendelea na matibabu ya jeraha la goti ambalo limekuwa likimsumbua mara kwa mara


"Kwa sasa ni mzima wa afya njema na nipo tayari kuitumikia timu yangu, unajua nilikuwa kwenye kipindi kigumu nilikuwa nasumbuliwa na majeraha sehemu ya mguu lakini baada ya kupata matibabu naona nipo vizuri na madaktari wameniruhusu kufanya mazoezi," alisema.


Moro amewataka mashabiki watarajie makubwa kwenye michezo iliyosalia kwani wachezaji wote wa klabu hiyo wanaendelea kufanya mazoezi makali kuandaa na mzunguko wa pili


Alisema akiwa kiongozi wa wachezaji atawahamasisha wenzake kucheza kwa kujituma kuisaidia timu na kuwafanya mashabiki wafurahi wakati wote


Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 44 katika michezo 18, ikishinda mechi 13, sare tano na inaendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo tangu ligi ya msimu huu ianze.

0 Comments:

Post a Comment