Saido: Tulieni tupige kaziiiii!


 STAA mpya wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wala hawapaswi kupaniki na maneno ya mitandaoni kwani wao wachezaji wanajua nini cha kufanya.


Saido ambaye ni raia wa Burundi ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara na Yanga. Wengine ni Mrundi mwenzie, Fiston Abdul Razak na mzawa, Dickson Job.


Straika huyo mzoefu na mechi kubwa amewasisitiza mashabiki wa Yanga kwamba mchezaji kutofunga siku moja isiwatishe bali waangalie ubora wake uwanjani na tachi zake zilivyo na macho na madhara makubwa.


“Watu wasivunjike moyo kwa matokeo ya mechi ya kirafiki, tutafanya vizuri kwenye mechi ijayo mbele yetu.Mashabiki wazidi kutusapoti sisi kila mechi kwetu itakuwa kama fainali,tutatumia akili na nguvu zetu zote kufikia kwenye malengo ambayo tunayahitaji,”alisema.


Kuhusu hali yake ya kiafya na kama atacheza mechi na Mbeya City alisema anaendelea vizuri na kadri siku zinavyoelekea atajua kama atacheza.


Ingawa Kocha wake, Cedrick Kaze alisema jana kwamba uwezekano wa kucheza Saido kwenye mechi ya wikiendi dhidi ya Mbeya ni hamsini kwa hamsini lakini kikosi chake kina wachezaji wengi wa kuamua matokeo.

0 Comments:

Post a Comment