Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) nchini Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa upimaji Darasa la nne, Kidato cha pili na Kidato cha nne.

Kwa urahisi unaweza kuyaona matokeo ya kidato cha NNE kwenye link iliyoandikwa ‘CSEE 2020’ >>> HAPA

Kwa urahisi unaweza kuyaona matokeo ya kidato cha PILI kwenye link iliyoandikwa ‘FTNA’ >>> HAPA

 

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 215, waliofanya udanganyifu katika upimaji wa mitihani hiyo, ambapo Darasa la Nne watahiniwa 77 wamefutiwa matokeo, kidato cha pili ni 63 na watahiniwa 75 wa kidato cha Nne.
"Kidato cha Nne somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili asilimia 94.83 likifuatiwa na Chemistry asilimia 87. 09 nafasi ya tatu ni Kingereza kwa asilimia 73.55 na Hisabati ikishika mkia kwa asilimia 20.12"- Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dkt Charles Msonde

"Kidato cha Nne waliofanya mitihani ni 434,654 waliofaulu ni 373,958 sawa na asilimia 85.84, ufaulu wa kidato cha nne umeongezeka kwa asilimia 5.19 ukilinganisha na mwaka 2019"- Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dkt Charles Msonde