Kaze aonyesha njia ya ubingwa


 KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema; “Tuna mechi 16 ili kumaliza msimu, katika mechi hizo tunatafuta pointi 48, hizi ni pointi nyingi sana katika Ligi yenye ushindani, sio kwa Yanga tu, hata Simba ambayo tunachuana nayo kwa karibu.”


Kaze alisema timu kama Azam na Biashara pia zina nafasi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa japo mashabiki wanaona zina pointi chache kulinganisha na za Simba au Yanga lakini yeye na vijana wake wanajua cha kufanya.


Biashara ni ya nne katika msimamo ikiwa na pointi 29 na Azam ina pointi 33 ikiwa ya tatu katika msimamo zote zina mechi 16 mkononi.


“Katika timu mechi 16 ni nyingi sana, japo lengo letu ni kuzishinda zote, ndiyo sababu tumeweka mikakati kila mechi kucheza kama fainali.


“Tunafanya hivi ili mwisho wa msimu tuone tumepata nini, kwani unaweza kucheza na kushinda mechi zote halafu ukakosa kile ambacho timu inakitarajia ikipate mwishoni mwa msimu,” alisema Kaze ambaye ni raia wa Burundi.


Kauli ya Kaze ni kama iko vichwani mwa mashabiki wa Yanga huko mitandaoni ambao wanawakebehi watani zao Simba kwamba hivi sasa kila mtu ashinde mechi zake zote ili mwishoni waone nani ataibuka bingwa.

0 Comments:

Post a Comment