Chikwende alikuwepo katika kikosi cha Platinums kilichotolewa na Simba kabla ya kutinga hatua za makundi.
INAWEZEKANA ikawa ni habari mbaya kwa mashabiki wa Simba baada ya kusikia winga wao machachari, Perfect Chikwende kutokuwa sehemu ya wachezaji watakaosafiri kwenda nchini DR Congo kucheza mechi ya hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.
Simba inaondoka leo, huku mchezaji huyo akikosekana kutokana na awali tayari alishacheza Ligi hiyo akiwa na kikosi cha FC Platinums.
Ikumbukwe kwamba katika hatua ya awali, Chikwende alicheza kwenye mchezo wa FC Platinums dhidi ya Simba na katika mchezo wa kwanza alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 uliopigwa nchini Zimbabwe.
Platinums licha ya kupata ushindi katika mchezo wa kwanza, walipokuja katika mchezo wa marudiano walifunga 4-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa na Platinums walitolewa na Simba waliingia katika hatua ya makundi.
Baada ya mechi hiyo Simba waliwekeza nguvu kuhakikisha wanaidaka saini ya mchezaji huyo na walifanikiwa kumpa mkataba wa miaka miwili.
0 Comments:
Post a Comment