Siku chache baada ya msanii kutoka lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny, kuachia albamu ya ‘The sound for Africa’ siku tano zilizopita sasa ni zamu ya Mbosso.
Mbosso ametangaza hilo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kwa kuandika’13th March Definition of love’.
Albamu hii itakuwa ya kwanza kwa msanii huyo kuitoa tangu alivyosainiwa katika lebo hiyo mwaka 2018 baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto ambalo alikuwa akifanya nalo kazi.
Tangu akiwa WCB ameshaachia vibao mbalimbali ikiwemo Watakubali, Nadekezwa, Alele,Maajabu, Sonona, Tamba,Nimekuozea,Ate,Nyota na sasa akitamba na kibao cha Fall.
Ujio wa abamu hii kwa mara ya kwanza msanii huyo alitangaza siku tatu zilizopita ambapo hata hivyo hakutaja tarehe zaidi ya kuwataka watu kutembelea kwenye youtube yake.
Ukiachilia mbali Mbosso ni kama WCB hapapoi kwani msanii mwingine kutoka lebo hiyo, Lavalava ametangaza ujio wa EP yake ambayo anatarajia kuiachia rasmi siku ya sikuu ya ‘Wapendanao’ Februari 14, 2021.
0 Comments:
Post a Comment