Kwa Tanzania wasanii waliokuwa wametajwa katika tuzo hizo ni Zuchu, Diamond Platnumz, Harmonize na kundi la Rostam.
Sherehe za utoaji tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2021 ambazo zilipangwa kufanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala zimeahirishwa.
Waandaaji tuzo hizo walitangaza jambo hilo jana Alhamisi Februri 4, 2012 kupitia mtandaao wao wa Twitter ambapo sherehe hiyo ilipaswa kufanyika Februari 20, 2021.
Kwa Tanzania wasanii waliokuwa wametajwa katika tuzo hizo ni msanii wa Bongo Fleva Zuchu aliyekuwa akiwania kipengele cha msanii chipukizi, Diamond Platanumz aliyekuwa akiwania kipengele cha msanii bora wa mwaka show kali kipindi cha ‘lockdown’,
Wengine ni Harmonize aliyekuwa akiwania kipingele cha msanii bora wa kiume na Rostam walikuwa wakiwania kipengele cha kundi bora la mwaka.
Hata hivyo pamoja na tangazo hilo la kuahirishwa, MTV haikutoa sababu zozote za kwa nini wameamua kukufanya hivyo.
Kufanyika kwa tuzo hizo Uganda,, ilikuwa ndio iwe mara ya kwanza kufanyika nchini humo na mara ya pili kufanyika katika nchi za Afrika Mashariki.
0 Comments:
Post a Comment